Mtindi na Asali katika matibabu ya chunusi

katika matumizi ya vipodozi asilia kwa utunzaji wa ngozi dhidi ya chunusi na bakteria ,leo tuangalie msaada wa mtindi na asali katika utunzaji wa ngozi hasa ile yenye chunusi.
Mtindi ni maziwa yaliyochachuka, yaani yanakuwa na asidi nyingi. Asidi ya kwenye mtindi ukitumika kwenye ngozi  ni kinga dhidi ya bakteria na yale mafuta yanasaidia kuleta unyevunyevu (moisturising)

MAHITAJI
  • Kijiko kimoja cha chakula cha Asali
  • Kijiko kimoja cha chakula cha mtindi 
  • Kipande cha pamba
JINSI YA KUFANYA
  • Changanya asali na mtindi uchanganyike vizuri
  •  Tumia kipande cha pamba kupaka usoni mchanganyiko wa asali na mtindi,hakikisha umepaka uso mzima
  • kaa kwa dakika 15 hadi 20
  • Sugua (scrub) taratibu  kuzunguka uso,kisha osha na maji safi
  • Paka mafuta yako unayotumia

No comments :

Post a Comment