APPLE CIDER VINEGAR INAVYOSAIDIA TATIZO LA CHUNUSI

Hakuna anayefurahia chunusi, na hakuna anayependeza akiwa na chunusi, Chunusi zimekuwa zikiwapata sana watu wenye ngozi za mafuta.Juhudi za kuteketeza mafuta yanayozidi kwenye ngozi zinahitajika kwani ndio chanzo kikuu cha chunusi.
Leo na waletea Apple cider vinegar (siki ya apple) kama kipodozi asilia cha kuzuia na kutibu chunusi.
Apple cider vinegar ina sifa ya kuua bakteria kwa haraka sana, pia ina sifa ya kukausha mafuta kwenye ngozi kwa haraka sana.Ila inashauriwa usitumie mara kwa mara maana kadri unavyokausha mafuta na apple cider vinegar ndivyo tezi za mafuta zinaongeza kasi ya kuzalisha mafuta yaliyokaushwa.

MAHITAJI

  • Siki ya apple (apple cider vinegar)
  • Maji safi
  • Pamba

MATUMIZI
  • Osha uso na maji safi,hakikisha uchafu wote umetoa
  •  changanya kifuniko kimoja cha siki kwa vifuniko vitatu vya maji
  • Chovya pamba kwenye mchanganyiko na upake maeneo yenye tatizo,kaa nayo kwa dakika 10 kisha osha,
  • Fanya hivyo mara nyingi uwezavyo kwa siku 
  • Pia unaweza kupaka na ukalala nayo usiku kucha 
  • Hakikisha unapaka moisturiser baada ya kutumia 

 

No comments :

Post a Comment