HOW TO GET RID OF STRETCH MARK?

Wapendwa nimekuwa adimu Sana,ila sasa nimerudi rasmi ile yenyewe.
 Stretch marks au michirizi ni matokeo ya kutanuka kwa ngozi,Mara nyingi hutokana na mimba,matumizi body cream Kali na hata ongezeko la mwili (unene).madukani kuna vipodozi vingi vya kupunguza michirizi ila nataka nikupe vipodozi mbadala ambavyo unaweza kutengeneza mwenyewe nyumbani.





1.KIAZI MBATATA 

Jinsi ya kufanya

Kata kiazi katika mtindo wa slice kisha sigua maeneo yenye michirizi kwa dakika 15 had I 20.acha kwa dakika 20 nyingine kisha osha kwa maji ya uvuguvugu.Fanya hivi mara tatu hadi nne kwa siku utapata matokeo mazuri haraka 


2.LIMAO NA BAKING SODA




Jinsi ya kufanya

Kata limao, chota baking soda kijiko kimoja changanya na kipande cha limao. Jipake mchanganyiko huku unasugua maeneo yenye michirizi kwa dakika 10 had I 15.Fanya hivi Mara tatu au zaidi kwa siku utafurahia matokeo

3.MAFUTA YA NAZI 

Jinsi ya kufanya

Paka mafuta ya nazi maeneo yenye michirizi kisha sugua ,paka Mara nyingi uwezavyo kwa siku. Unaweza kuchanganya mafuta ya Nazi na   mafuta ya zaituni(olives oil),mafuta ya alizeti,cocoa butter,shear butter na mafia ya parachichi


4.ALOE VERA (MSHUBIRI)


 Jinsi ya kufanya

 Kata jani aloe vera paka utomvu wake  kwenye  michirizi kisha fugue kwa dakika  10 hadi 15 kisha osha kwa maji  ya uvuguvugu .Baada ya wiki tatu utajifurahia

 ZINGATIA ,katika utunzaji ngozi ili ufanikiwe kunywa maji mengi,mbogamboga na  matunda ni jambo la msingi S Ni  matumaini yangu ukifuata  matumizi Kama nilivyoelekeza utapata matokeo mazuri ndani ya wiki tatu hadi  mwezi.

Tukutane kesho  👋👋👋👋






























































































































No comments :

Post a Comment