Visunzua ni vinyama vidogovidogo vinavyoota juu ya ngozi, hili ni tatizo la watu wengi kwa sasa, wanawake na wanaume huwatokea. Inasemekana visunzua hutokana na tatizo la homoni mwilini, unene uliopitiliza, kisukari na mabadiliko wakati wa mimba.Watu wengi wanahangaika kutafuta tiba ya visunzua bila mafanikio. Nitakueleza vitu ambavyo unaweza kuandaa mwenyewe nyumbani kukabiliana na tatizo hili na likaisha ndani ya muda mfupi. Vitu vingine ukivisoma hapa utastaajabu maana huwezi kufikiria vinaweza kuwa tiba
1.KITUNGUU MAJI NA APPLE CIDER
Kata vitunguu katika slice weka kwenye bakuli ,changanya na apple cider kisha viache vilowane usiku kucha,asubuhi chukua vitunguu bandika kwenye visunzua kisha funga vizuri na plasta visitoke acha kwa masaa 4 hadi matano.Fanya hivi kila siku kwa muda wa wiki moja utajipenda
2.KITUNGUU SAUMU,BAKING SODA NA LIMAO
Menya kitunguu saumu ,kisage kiwe laini changanya na baking soda kijiko kimoja kisha changanya na limao.Paka mchanganyiko kwenye sunzua ukiweza funga na plasta,kaa kwa masaa mawili hadi matatu osha. Paka mara 3 kwa siku. Ni vizuri usiku ukilala nayo. Baada ya muda mfupi utapata matokeo mazuri
3.ASPIRIN
Yes ile aspirin dawa ambayo humezwa Kwa kutuliza maumivu, hapa huimezi.unaiponda upate unga kisha changanya na matone ya maji ilainike.paka kwenye sunzua Mara tatu hadi nne kwa siku. Baada ya wiki utajifurahia
4.RANGI YA KUCHA
Sio tu urembo was kucha ,hapa rangi inafanya kazi nyingine.paka rangi kwenye sunzua mara tatu hadi nne kwa siku.usiku unashauriwa kulala nayo na ubandue asubuhi.wiki moja tuu njoo unipe feedback
5.GANDA LA NDIZI
Bandika sehemu ya ndani ya ganda la ndizi na usugue kwenye sunzua Mara nyingi uwezavyo kwa siku .ili upate matokeo mazuri bandika plasta na uiache kwa muda mrefu.
Kupitia article yangu ya Leo ni matarajio yangu kuna kitu kipya umejifunza na hilo ndio lengo la kijiwe hiki, usisite kuniandikia maoni yako kwenye email yangu dondosha comment hapo chini
Karibu katika kijiwe hiki cha MarhabaaZanzibar ili tubadilishane uzoefu kuhusu maisha yetu ya kiafrika, tutakuwa na utunzaji ngozi,mavazi, vyakula ,matukio,upashanaji habari na mtindo wa maisha halisi ya kiafrika hususan Zanzibar Ni matarajio yangu kujifunza zaidi kupitia nyinyi wasomaji wangu,nanyi nina imani hamtakosa cha kujifunza toka kwangu. Karibuni sanaaa
Hakika Leo nimejua kitu kipya kabisa Mungu awabarik Sana kwa somo hili
ReplyDeleteasanteeee
ReplyDeleteHabari,je hii natumia hata Kama vipo katika uchi dct?
ReplyDeletenipigie sasa +255743564170
DeleteKama vimekutoka uso mzima je unaweza paka rangi ya kucha uso wote??
ReplyDeletethanx
ReplyDeleteLazima kuweka plasta?
ReplyDelete