Jumatatu huwa inakuwa siku ya hekaheka Sana ,maana mipango ya wiki nzima inaanzia hapa,ukichanganya na uchovu was weekend basi ndio kabisaa siku inakuwa haitoshi.kwa hiyo jumatatu tuwe tunavumiliana nitakuwa naandika kidogo Sana pia itakuwa kama hivi leo nachelewa kuweka andiko.
Leo nimekuja na urembo unaotesa wanawake wengi mpaka wanahangaika kuweka za kununua,lol. Kope ni moja ya kivutio katika uso,ndio maana watu wanahangaika kuweka za bandia.Kitu kibaya kwenye kope za bandia ukiweka muda mrefu unapoteza hata zile chache ulizokuwa nazo mwanzoni.Hii sio tu kwa wanaotaka kujaza nope bali hata wale kope zao zimeharibiwa na matumizi ya kope bandia.
MAAJABU YA VASELINE KATIKA KUKUZA NA KUJAZA KOPE
Naiongelea ile Vaseline blue seal ambayo wengi tunatumia kupaka kwenye ngozi.Kwenye kukuza na kujaza kope paka Vaseline kwenye kope zako kila siku jioni kabla ya kulala.Baada ya wiki mbili hadi tatu utaona mabadiliko.
Leo ni hayo tuu, tukutane kesho
Karibu katika kijiwe hiki cha MarhabaaZanzibar ili tubadilishane uzoefu kuhusu maisha yetu ya kiafrika, tutakuwa na utunzaji ngozi,mavazi, vyakula ,matukio,upashanaji habari na mtindo wa maisha halisi ya kiafrika hususan Zanzibar Ni matarajio yangu kujifunza zaidi kupitia nyinyi wasomaji wangu,nanyi nina imani hamtakosa cha kujifunza toka kwangu. Karibuni sanaaa
Kama ni ukwelii nitakushukuru sana
ReplyDelete