PATA NGOZI MTELEZO (FLAWLESS SKIN)

Kuna watu ni wazuri jamani ila uzuri wao hauonekani sababu ngozi zao zipo rough sana, ubora  wa ngozi ni matokeo ya mambo mengi Sana ,najua kufanya yote kwa sisi tulio busy ni ngumu kidogo ,ila ukifanya japo mawili matatu utanawirika tu.Nakukumbusha mambo hayo ya msingi ni  kula vizuri mbogamboga na matunda,kunywa maji mengi na kusafisha uso kwa vitu asilia angalau mara moja kwa wiki. Zipo njia nyingi sana za kusafisha ngozi kiasili.Leo nitakupa moja na ukiifanya ipasavyo haitokuangusha.Nitatenganisha jinsi ya kusafisha ngozi ya mafuta na zile ngozi za kawaida na kavu.Kama huijui aina ya ngozi yako ,andiko linalifuata litakuwa jinsi ya kuitambua aina ya ngozi yako.
KWA NGOZI YA MAFUTA
Mahitaji
-Ute wa yai
-kipande cha  limao
-manjano kijiko kimoja

.Jinsi ya kufanya
Changanya vitu vyote katika chombo kimoja,kisha osha uso na sabuni isiyo na kemikali ,jikaushe kisha paka mchanganyiko wako usoni.kaa nao kwa dakika 20 hadi 30 kisha osha.
Ili kuzuia ngozi isiwe kavu Sana ,paka moisturizer unayotumia.

KWA NGOZI KAVU NA YA KAWAIDA
Mahitaj:
-Kiini cha yai
-maziwa fresh
-Manjano kijiko kimoja

Jinsi ya kufanya :

Changanya vitu vyote katika chombo kimoja,kisha osha uso na sabuni isiyo na kemikali ,jikaushe kisha paka mchanganyiko wako usoni.kaa nao kwa dakika 20 hadi 30 kisha osha.
Ili kuzuia ngozi isiwe kavu Sana ,paka moisturizer unayotumia.
 Wadau kwa leo ni haya,tukutane wakati mwingine kwa mada nyingine

No comments :

Post a Comment