Hapo zamani tulizoea kuiona manjano jikoni tuu, mchuzi bila manjano au wengine wanaita binzari msosi ulikuwa haujanoga bado. Siku hizi mambo yamebadilika manjano imekuwa kiungo muhimu katika ngozi,bila manjano urembo wako haujakamilika.kwenye meza yako ya vipodozi hakikisha Una kikopo cha manjano.Manjano ninayoongelea hapa ni Ile manjano mbichi haijazimuliwa na sembe.maana unaweza ukanunua manjano kumbe wajanja washakuchezea akili.Manjano halisi tena ile fresh ambayo haijakaa muda mrefu store .Hapa tuzianagalie faida na jinsi ya kufanya kufikia matarajio.
1.Inatibu chunusi
Kutokana na tabia uake ya kupambana na bakteria manjano inauwezo wa kukausha chunusi hasa zile zinazotokana na maambukizi ya bakteria. Kwa wenye ngozi ya mafuta unachanganya manjano na m aji ya waridi na wale wenye ngozi kavu unachanganya manjano na mziwa fresh kisha unapaka usoni kwa nusu saa kisha unaosha na maji ya kawaida
2. Inang'arisha ngozi
Manjano inatabia ya kutoa weusi kwenye ngozi unaotokana na cream,kuungua jua au kufubaa kwa ngozi. Changanya manjano na maji ya waridi kisha sugua sehemu iliyoathirika.
3.Inapunguza mikunjo ya uzee.
Kwa wale wenzangu na miyee "age go" manjano ni kimbilio letu. Inapunguza Ile mistari na mikunjo inayoletwa na umri mkubwa.Unachanganya manjano na mtindi na kupaka kwenye ngozi kwa nusu saa.
4.Inapunguza mafuta
Kwa wenye ngozi ya mafuta manjano inasaidia sana kupunguza uzalishaji we mafuta,hapa mtashanga kidogo, Unakunywa glass moja ya mchanganyiko wa maji na manjano angalau mara mbali kwa wiki. Pia unaweza kuchanganya manjano,limao na maji ya waridi na kupaka usoni kwa dakika 30
5.Inapunguza kasi ya ngozi kuzeeka
Baada ya matumizi ya make up wiki nzima jitahidi mwisho wa wiki uwe unafanya facial ya manjano angalau mara moja,maana manjano husaidia ngozi isichoke haraka na hivyo kupaka mwonekano mzuri wa ngozi yako.
Karibu katika kijiwe hiki cha MarhabaaZanzibar ili tubadilishane uzoefu kuhusu maisha yetu ya kiafrika, tutakuwa na utunzaji ngozi,mavazi, vyakula ,matukio,upashanaji habari na mtindo wa maisha halisi ya kiafrika hususan Zanzibar Ni matarajio yangu kujifunza zaidi kupitia nyinyi wasomaji wangu,nanyi nina imani hamtakosa cha kujifunza toka kwangu. Karibuni sanaaa
Asante sana
ReplyDelete