Karibuni kijiweni wadau,
Leo tuangalie hili tatizo la sugu maana limekuwa kubwa katika ulimwengu wa warembo, hasa wale team "natural iachie misitu '' ha ha haa.
Jambo kubwa kufahamu kabla hujaanza kuzitafutia tiba ni kujua chanzo cha tatizo lako.
Mara nyingi sugu husababishwa na matumizi ya cream kali hasa zenye hydroquinnone, ukavu wa ngozi, magonjwa ya ngozi, utunzaji mbaya wa ngozi na pia wengine ni maumbile yao.
Sugu hutokea kwenye vidole vya mikono,miguu,viwiko vya mikono na kwenye magoti.
Kwa sababu zote nilizotaja zinarekebishika labda hiyo ya maumbile. Tuone jinsi unaweza kulimaliza mwenyewe nyumbani kwa kuandaa vitu asilia visivyo na kemikali.
1.Kiazi mbatata, limao na baking soda
Kata kiazi katika vipande vidogo kisha sugua kwenye sugu, bila kuosha chukua kijiko kimoja cha baking soda changanya na limao upate paste nzito. Paka kwenye sugu kisha sugua taratibu kwa dakika 10, fanya hivi usiku kabla ya kulala mpaka utakaporidhika na matokeo
2.Limao na sukari
Changanya kijiko kimoja cha sukari na kipande cha limao (kamua upate juisi) ,paka mchanganyiko wako kwenye sugu kisha sugua kwa dakika 15 hadi 20. Fanya hivi kila siku usiku kabla ya kulala mpaka utakaporidhika na matokeo
Leo tuishie hapa ,usisahau kuniandikia maoni yako au maswali kwenye comment hapo chini
Karibu katika kijiwe hiki cha MarhabaaZanzibar ili tubadilishane uzoefu kuhusu maisha yetu ya kiafrika, tutakuwa na utunzaji ngozi,mavazi, vyakula ,matukio,upashanaji habari na mtindo wa maisha halisi ya kiafrika hususan Zanzibar Ni matarajio yangu kujifunza zaidi kupitia nyinyi wasomaji wangu,nanyi nina imani hamtakosa cha kujifunza toka kwangu. Karibuni sanaaa
No comments :
Post a Comment