NYWELE ZAKO ZINAKATIKA?

Leo tupo na urembo wa nywele, nywele inaongeza haiba,mvuto katika mwonekano wa  mtu. Ila mvuto wa  nywele hauji hivihivi.unahitaji matunzo na kujitoa kikwelikweli. Na katika Dunia  ya Leo bidhaa za utunzaji nywele ni gharama sana. Huna haja ya kuwaza gharama za utunzaji nywele wala huna haja ya kujipa hofu ya kubaki kinyonyoke.ha ha haaa.
 Leo nitakupa steaming za asili utafanya mwenyewe nyumbani na utasahau habari za uwaraza bila kutumia gharama nyingi.

1.Kitunguu maji

Unahitaji kuwa na kitunguu maji kikubwa ,utakisaga na maji kidogo Sana upate juisi nzito.paka kwenye mashina ya nywele kisha vaa kofia ya plastiki acha kwa nusu saa hadi lisaa limoja,Fanya hivi mara moja kwa wiki kwa muda wa mwezi mmoja tuu tatizo linaisha.ila nywele zitanuka Sana,si mnajua harufu ya kitunguu

2.Kiazi mbatata

Kwenye urembo hiki tunakutana nacho sehemu nyingi, saga kiazi kilainike kikiwa kibichi.pakaa kichwani na uvae kofia ya plastick kwa SAA 1 .Fanya Mara 1 kwa wiki kwa muda wa mwezi mmoja.
 3.Spinach na ute was yai

Saga majani ya spinach changanya na ute wa yai bila kiini, paka kwenye nywele zote. Vaa kofia ya plastiki kwa saa 1.kisha OSHA.Fanya hivi Mara moja kwa wiki

4.Kula vizuri

Jitahidi katika mlo wako kuwe na vyakula Kama mboga za majani,samaki wa baharini,karanga/korosho,parachichi ,mayai n.k


No comments :

Post a Comment