Watu wanajisahau Sana siku hizi, make up zimekuwa ndio maisha yetu.Tunasahau kuna muda hatupaki make up .Kitu cha kuzingatia make up isiwe ndio wewe ,ndio kila kitu.Hata bila make up unatakiwa uwe unajiamini kuwa ni mrembo wa haja.
Leo tuone urembo wa lips ,jinsi ya kutunza lips.Unahitaji kufanya scrub lips zako Mara kwa Mara ili kuondoa ngozi iliyokufa. Scrub ya lips sio Kama ya uso maana ngozi ya lips in laini name rahisi kupata madhara.
Mahitaji: sukari,mafuta ya nazi na asali
Jinsi ya kufanya : weka mafuta ya Nazi kwenye freezer mpaka yawe magumu wastani, kisha changanya na asali ichanganyike vizuri.malizia kuchanganya na sukari .
Paka kwenye lips zako huku unasugua taratibu.Fanya scrub angalau Mara moja kwa wiki.
Baada ya kutumia scrub yako hifadhi kwenye fridge ili isipoteze ubora
Karibu katika kijiwe hiki cha MarhabaaZanzibar ili tubadilishane uzoefu kuhusu maisha yetu ya kiafrika, tutakuwa na utunzaji ngozi,mavazi, vyakula ,matukio,upashanaji habari na mtindo wa maisha halisi ya kiafrika hususan Zanzibar Ni matarajio yangu kujifunza zaidi kupitia nyinyi wasomaji wangu,nanyi nina imani hamtakosa cha kujifunza toka kwangu. Karibuni sanaaa
No comments :
Post a Comment