RAFIKI MKIA WA FISI


Hii sio story ya kutunga,ni kweli imetokea, kuna huyu Dada alikuwa na mpenzi wake anaishi Uingereza ,walikuwa mbali ila mapenzi yapo. Mwezi  wa kumi mwaka Jana huyu  Dada kaenda kumtembea shoga yake,kwa bahati mpenzi wake wa UK akamskype wakaanza kupiga story.Jamaa akamuuliza kwani Leo upo  wapi,bibiye akajibu nipo kwa shoga yangu.Jamaa akaomba amuone shogake ili ajiridhishe Kama yupo huko kweli, mdada akaelekeza camera kwa rafiki yake aonwe na mpenzi wake.Baada ya maongezi ya Skype kuisha jamaa akatuma msg kuwa rafiki yake walikuwa wote wakati anaongea amemuona shogake hivyo anaomba mawasiliano yake.Bi Dada akamuiliza shogake Kama yupo tayari kuwasiliana na rafiki wa mpenzi wake,akakubali.Bila hiyana Dada wa watu akatuma namba kwa mpenzi wake ili ampe rafiki yake.
Basi  bwana hazijapita hata siku mbili jamaa mwenyewe akajitosa kuwasiliana na shoga wa mpenzi wake(namba aliitaka yeye akasingizia anataka rafiki yake). Siku zinaenda mawasiliano yamepamba moto mpaka kufika mwezi was 12 jamaa akarudi Afrika kimyakimya kaja kumchumbia shoga wa mpenzi wake.Baada ya kumaliza kilichomleta jamaa akamtafuta yule bi dada wa mwanzo  akiwa na huyo alomchumbia.Dada hana  hili wala lile akajua sweetheart kaja kimya kimya amenisurprise, kufika Kule akakutana na surprise ya kikwelikweli,akatambulishwa na jamaa eti "huyu ndiye aliyenileta,nimekuja kumchumbia" kwa hiyo Mimi na wewe baaasi.Bi Dada hajaamini kajiliza weee .Na hizo convo hapo juu ni kati ya bidada na shogake baada ya sekeseke.

Ungekuwa wewe ungefanyaje?

No comments :

Post a Comment