Mara nyingi weusi wa kuzunguka jicho husababishwa na umri
mkubwa,ngozi kavu,tabia ya kulia mara kwa mara,msongo wa mawazo(stress) ,kukosa
usingizi, mlo mbaya usiozingatia afya ,kurithi na matumizi ya cream kemikali
kali.
Sasa tuone unaandaje tiba ya tatizo hili ukiwa mwenyewe
nyumbani
1.Tango na juisi ya limao
Kata tango na ulisage lilainike,kamulia na nusu kipande cha limao. Paka mchanganyiko wako
wakati wa kulala na usioshe hadi asubuhi utakapoamka.Hakikisha unaosha na maji
ya baridi.Itakuwa vizuri zaidi kama utapaka na asubuhi kwa dakika kama 15 kisha
utaosha .Ndani ya wiki moja tarajia kuona mabadiliko kwa tiba hii
2.Nyanya na limao
Saga nyanya changanya na juisi ya limao nusu kipande, chukua
pamba ichovye kwenye mchanganyoko kisha iweke kuzunguka jicho (lala chali)
hakikisha miwani yote imezibwa.fanya hivi mara mbili kwa siku kwa matokeo mazuri
Saka kiazi kibichi ,kasha chovya pamba kwenye juisi ya kiazi
na uweke kuzunguka jicho,hakikisha weusi wote umezibwa.fanya hivi mara mbili
kwa siku mpaka utakapopata matokeo ya kuridhisha
4.Rose water/ Maji ya waridi
Hii rose wate hata kama huna weusi kuzunguka jicho ni mazuri
kupakaa mara kwa mara machoni kujikinya na kupoteza mwonekano wa uso wa
wako.Chovya pamba kwenye rose water kishaweka kuzunguka jicho kwa dakika 15
hadi 20,huna haja ya kunawa.utapaka asubuhi na jioni kwa matokeo mazuri
No comments :
Post a Comment