Chunusi ni tatizo linalosumbua wengi, si wanawake si wanaume ,yaani halichagui jinsia.
Chunusi zinaweza kusabishwa na wingi wa tezi za mafuta kwenye ngozi, vyakula tunavyokula hasahasa sukari, mafuta mafuta na chumvi wakati mwingine.vyakula vinavyotajwa sana ni vile vyenye wanga sana kama chipsi na vyakula vya fast food mara nyingi wanatumia iodised salt kupikia.
Sasa tuone vitu mbalimbali asilia vinavyoweza kukusaidia katika tatizo la chunusi,ambavyo ni rahisi kufanya mwenyewe nyumbani.
1.Kitunguu thomu (garlic)
Sugua eneo lenye chunusi au kovu la chunusi kwa punje ya kitunguu thomu, mara nyingi uwezavyo kwa siku
Fanya hivi kwa siku kadhaa chunusi zitaisha.
2. Majani ya Muarobaini ( Neem)
Osha majani ya muarobaini kiasi kidogo, yasage kwenye blenda kisha nawa uso mara 3 kwa siku, kwa siku kadhaa utaona mabadiliko
Au unaaweza kuosha majani ya muarobaini ,kisha yachemshe weka uso wako juu ya mvuke kwa dakika 5 hadi 10 mara 3 kwa siku.Fanya hivi kwa siku kadhaa utaona mabadiliko
3.Limao (lemon)
Osha uso wako vizuri, kamua limao lako upate juice kisha chukua kipande cha pamba anza kupaka usoni.
Njia nyingine unaweza kuchemsha maji ya moto ,weka uso wako ili upatwe na mvuke maji yanapochemka, bada ya hapo kata limao lako kamua upate juisi, chukua pamba chovya kwenye juisi na upake usoni.
Fanya hivi mara 2 kwa wiki au mara 1 kwa siku kwa siku 7 kutegemea na ukubwa wa tatizo.
4.Aloe Vera
Saga majani ya aloe vera upate uji mzito ,osha uso wako vizuri kisha paka uji wa aloe vera usoni, kaa nao kwa dakika 10 hadi 15 kisha osha
Fanya hivi mara 1 hadi 2 kwa wiki utafurahia matokeo.
Karibu katika kijiwe hiki cha MarhabaaZanzibar ili tubadilishane uzoefu kuhusu maisha yetu ya kiafrika, tutakuwa na utunzaji ngozi,mavazi, vyakula ,matukio,upashanaji habari na mtindo wa maisha halisi ya kiafrika hususan Zanzibar Ni matarajio yangu kujifunza zaidi kupitia nyinyi wasomaji wangu,nanyi nina imani hamtakosa cha kujifunza toka kwangu. Karibuni sanaaa
No comments :
Post a Comment