Mrembo mwenye vipaji vingi Jokate akiwa na stylist Joel

NYWELE ZAKO ZINAKATIKA?

Leo tupo na urembo wa nywele, nywele inaongeza haiba,mvuto katika mwonekano wa  mtu. Ila mvuto wa  nywele hauji hivihivi.unahitaji matunzo na kujitoa kikwelikweli. Na katika Dunia  ya Leo bidhaa za utunzaji nywele ni gharama sana. Huna haja ya kuwaza gharama za utunzaji nywele wala huna haja ya kujipa hofu ya kubaki kinyonyoke.ha ha haaa.
 Leo nitakupa steaming za asili utafanya mwenyewe nyumbani na utasahau habari za uwaraza bila kutumia gharama nyingi.

1.Kitunguu maji

Unahitaji kuwa na kitunguu maji kikubwa ,utakisaga na maji kidogo Sana upate juisi nzito.paka kwenye mashina ya nywele kisha vaa kofia ya plastiki acha kwa nusu saa hadi lisaa limoja,Fanya hivi mara moja kwa wiki kwa muda wa mwezi mmoja tuu tatizo linaisha.ila nywele zitanuka Sana,si mnajua harufu ya kitunguu

2.Kiazi mbatata

Kwenye urembo hiki tunakutana nacho sehemu nyingi, saga kiazi kilainike kikiwa kibichi.pakaa kichwani na uvae kofia ya plastick kwa SAA 1 .Fanya Mara 1 kwa wiki kwa muda wa mwezi mmoja.
 3.Spinach na ute was yai

Saga majani ya spinach changanya na ute wa yai bila kiini, paka kwenye nywele zote. Vaa kofia ya plastiki kwa saa 1.kisha OSHA.Fanya hivi Mara moja kwa wiki

4.Kula vizuri

Jitahidi katika mlo wako kuwe na vyakula Kama mboga za majani,samaki wa baharini,karanga/korosho,parachichi ,mayai n.k


MAMBO YA KUWEKA PICHA YA BAE KWENYE MITANDAO ANGALIA YASIKUKUTE HAYA



  Kwa ambao hawajaelewa,kuna bi dada huko Nigeria kaweka picha Instagram yupo na jamaa akaandika ndo bae wake, jamaa kuiona akaja juu picha ifutwe yeye sio bae wake hehehee. Dada akamyuti kama siku mbili hivi (nadhani aibu ,kuzodolewa mbele ya kadamnasi sio jambo dogo) akaja na utetezi eti jamaa alimwambia ametalikiana na mkewe ,hivyo yupo single ,wakadate muda mrefu mpaka siku anaweka ile picha walikuwa wamekorofishana ,kwahiyo hata jamaa alipomkana zilikuwa hasira.pia hakujua  Kama jamaa ana make.

Aibu kama hizi sio nzuri mweeh! Kwani lazma na we we uonekane Una bae? Post hata nyau ila sio mtu hujui mko wangapi

JINSI YA KUKABILIANA NA WEUSI KUZUNGUKA JICHO (DARK CIRCLE)



Mara nyingi weusi wa kuzunguka jicho husababishwa na umri mkubwa,ngozi kavu,tabia ya kulia mara kwa mara,msongo wa mawazo(stress) ,kukosa usingizi, mlo mbaya usiozingatia afya ,kurithi na matumizi ya cream kemikali kali.

Sasa tuone unaandaje tiba ya tatizo hili ukiwa mwenyewe nyumbani
1.Tango na juisi ya limao

Kata tango na ulisage lilainike,kamulia na  nusu kipande cha limao. Paka mchanganyiko wako wakati wa kulala na usioshe hadi asubuhi utakapoamka.Hakikisha unaosha na maji ya baridi.Itakuwa vizuri zaidi kama utapaka na asubuhi kwa dakika kama 15 kisha utaosha .Ndani ya wiki moja tarajia kuona mabadiliko kwa tiba hii
2.Nyanya na limao

Saga nyanya changanya na juisi ya limao nusu kipande, chukua pamba ichovye kwenye mchanganyoko kisha iweke kuzunguka jicho (lala chali) hakikisha miwani yote imezibwa.fanya hivi mara mbili kwa siku kwa matokeo mazuri
3.Kiazi mbatata
Saka kiazi kibichi ,kasha chovya pamba kwenye juisi ya kiazi na uweke kuzunguka jicho,hakikisha weusi wote umezibwa.fanya hivi mara mbili kwa siku mpaka utakapopata matokeo ya kuridhisha
4.Rose water/ Maji ya waridi
Hii rose wate hata kama huna weusi kuzunguka jicho ni mazuri kupakaa mara kwa mara machoni kujikinya na kupoteza mwonekano wa uso wa wako.Chovya pamba kwenye rose water kishaweka kuzunguka jicho kwa dakika 15 hadi 20,huna haja ya kunawa.utapaka asubuhi na jioni kwa matokeo mazuri

PATA NGOZI MTELEZO (FLAWLESS SKIN)

Kuna watu ni wazuri jamani ila uzuri wao hauonekani sababu ngozi zao zipo rough sana, ubora  wa ngozi ni matokeo ya mambo mengi Sana ,najua kufanya yote kwa sisi tulio busy ni ngumu kidogo ,ila ukifanya japo mawili matatu utanawirika tu.Nakukumbusha mambo hayo ya msingi ni  kula vizuri mbogamboga na matunda,kunywa maji mengi na kusafisha uso kwa vitu asilia angalau mara moja kwa wiki. Zipo njia nyingi sana za kusafisha ngozi kiasili.Leo nitakupa moja na ukiifanya ipasavyo haitokuangusha.Nitatenganisha jinsi ya kusafisha ngozi ya mafuta na zile ngozi za kawaida na kavu.Kama huijui aina ya ngozi yako ,andiko linalifuata litakuwa jinsi ya kuitambua aina ya ngozi yako.
KWA NGOZI YA MAFUTA
Mahitaji
-Ute wa yai
-kipande cha  limao
-manjano kijiko kimoja

.Jinsi ya kufanya
Changanya vitu vyote katika chombo kimoja,kisha osha uso na sabuni isiyo na kemikali ,jikaushe kisha paka mchanganyiko wako usoni.kaa nao kwa dakika 20 hadi 30 kisha osha.
Ili kuzuia ngozi isiwe kavu Sana ,paka moisturizer unayotumia.

KWA NGOZI KAVU NA YA KAWAIDA
Mahitaj:
-Kiini cha yai
-maziwa fresh
-Manjano kijiko kimoja

Jinsi ya kufanya :

Changanya vitu vyote katika chombo kimoja,kisha osha uso na sabuni isiyo na kemikali ,jikaushe kisha paka mchanganyiko wako usoni.kaa nao kwa dakika 20 hadi 30 kisha osha.
Ili kuzuia ngozi isiwe kavu Sana ,paka moisturizer unayotumia.
 Wadau kwa leo ni haya,tukutane wakati mwingine kwa mada nyingine























































JINSI YA KUKABILIANA NA SUGU

Karibuni kijiweni wadau,
 Leo tuangalie hili tatizo la sugu maana limekuwa kubwa katika ulimwengu wa  warembo, hasa wale team "natural iachie misitu '' ha ha haa.
 Jambo kubwa kufahamu kabla hujaanza kuzitafutia tiba ni kujua chanzo cha tatizo lako.
Mara nyingi sugu husababishwa na matumizi ya cream kali hasa zenye hydroquinnone,  ukavu wa ngozi, magonjwa ya ngozi, utunzaji mbaya wa ngozi na pia wengine ni maumbile yao.
Sugu hutokea kwenye vidole vya mikono,miguu,viwiko vya mikono na kwenye magoti.
Kwa sababu zote nilizotaja zinarekebishika labda hiyo ya maumbile. Tuone jinsi unaweza kulimaliza mwenyewe nyumbani kwa kuandaa vitu asilia visivyo na kemikali.



 1.Kiazi mbatata, limao na baking soda
 Kata kiazi katika vipande vidogo kisha sugua kwenye sugu, bila kuosha chukua kijiko kimoja cha baking soda changanya na limao upate paste nzito. Paka kwenye sugu kisha sugua taratibu kwa dakika 10, fanya hivi usiku kabla ya kulala mpaka utakaporidhika na matokeo

2.Limao na sukari
Changanya kijiko kimoja cha sukari na kipande cha limao (kamua upate juisi) ,paka mchanganyiko wako kwenye sugu kisha sugua kwa dakika 15 hadi 20. Fanya hivi kila siku usiku kabla ya kulala mpaka utakaporidhika na matokeo

Leo tuishie hapa ,usisahau kuniandikia maoni yako au maswali kwenye comment hapo chini 



JINSI YA KUJAZA NA KUREFUSHA KOPE ZAKO

Jumatatu huwa inakuwa siku ya hekaheka Sana ,maana mipango ya wiki nzima inaanzia hapa,ukichanganya na uchovu was weekend basi ndio kabisaa siku inakuwa haitoshi.kwa hiyo jumatatu tuwe tunavumiliana nitakuwa naandika kidogo Sana pia itakuwa kama hivi leo nachelewa kuweka andiko.
 Leo nimekuja na urembo unaotesa wanawake wengi mpaka wanahangaika kuweka za kununua,lol. Kope ni moja ya kivutio katika uso,ndio maana watu wanahangaika kuweka za bandia.Kitu kibaya kwenye kope za bandia ukiweka muda mrefu unapoteza hata zile chache ulizokuwa nazo mwanzoni.Hii sio tu kwa wanaotaka kujaza nope bali hata wale kope zao zimeharibiwa na matumizi ya kope bandia.

MAAJABU YA VASELINE KATIKA KUKUZA NA KUJAZA KOPE



Naiongelea ile Vaseline blue seal ambayo wengi tunatumia kupaka kwenye ngozi.Kwenye kukuza na kujaza kope paka Vaseline kwenye kope zako kila siku jioni kabla ya kulala.Baada ya wiki mbili hadi tatu utaona mabadiliko.



Leo ni hayo tuu, tukutane kesho


GET RID OF SKIN TAGS/WARTS (VISUNZUA)

Visunzua ni vinyama vidogovidogo vinavyoota juu ya ngozi, hili ni tatizo la watu wengi kwa sasa, wanawake na wanaume huwatokea. Inasemekana visunzua hutokana na tatizo la homoni mwilini, unene uliopitiliza, kisukari na mabadiliko wakati wa  mimba.Watu wengi wanahangaika kutafuta tiba ya visunzua bila mafanikio. Nitakueleza vitu ambavyo unaweza kuandaa mwenyewe nyumbani kukabiliana na tatizo hili na likaisha ndani ya muda mfupi. Vitu vingine ukivisoma hapa utastaajabu  maana huwezi kufikiria vinaweza kuwa tiba








1.KITUNGUU MAJI NA APPLE CIDER





Kata vitunguu katika slice weka kwenye bakuli ,changanya na apple cider kisha viache vilowane usiku kucha,asubuhi chukua vitunguu bandika kwenye visunzua kisha funga vizuri na plasta visitoke acha kwa masaa 4 hadi matano.Fanya hivi kila siku kwa muda wa wiki moja utajipenda





2.KITUNGUU SAUMU,BAKING SODA NA LIMAO


Menya kitunguu saumu ,kisage kiwe laini changanya na  baking soda kijiko kimoja kisha changanya na limao.Paka mchanganyiko kwenye sunzua ukiweza funga na  plasta,kaa kwa masaa mawili hadi matatu osha. Paka mara 3 kwa siku. Ni vizuri usiku ukilala nayo. Baada ya muda mfupi utapata matokeo mazuri


 3.ASPIRIN


Yes ile aspirin dawa ambayo humezwa Kwa kutuliza maumivu, hapa huimezi.unaiponda upate  unga kisha changanya na matone ya maji ilainike.paka kwenye sunzua Mara tatu hadi nne kwa siku. Baada ya wiki utajifurahia


 4.RANGI YA KUCHA




Sio tu urembo was kucha ,hapa rangi inafanya kazi nyingine.paka rangi kwenye sunzua mara tatu hadi nne kwa siku.usiku unashauriwa kulala nayo na ubandue asubuhi.wiki moja tuu njoo unipe feedback

5.GANDA LA NDIZI

Bandika sehemu ya ndani ya ganda la ndizi na usugue kwenye sunzua Mara nyingi uwezavyo kwa siku .ili upate matokeo mazuri bandika plasta  na uiache kwa muda mrefu.







Kupitia article yangu  ya Leo ni matarajio yangu kuna kitu kipya umejifunza na hilo ndio lengo  la kijiwe hiki, usisite  kuniandikia maoni yako kwenye email yangu  dondosha comment hapo chini


HOW TO GET RID OF STRETCH MARK?

Wapendwa nimekuwa adimu Sana,ila sasa nimerudi rasmi ile yenyewe.
 Stretch marks au michirizi ni matokeo ya kutanuka kwa ngozi,Mara nyingi hutokana na mimba,matumizi body cream Kali na hata ongezeko la mwili (unene).madukani kuna vipodozi vingi vya kupunguza michirizi ila nataka nikupe vipodozi mbadala ambavyo unaweza kutengeneza mwenyewe nyumbani.





1.KIAZI MBATATA 

Jinsi ya kufanya

Kata kiazi katika mtindo wa slice kisha sigua maeneo yenye michirizi kwa dakika 15 had I 20.acha kwa dakika 20 nyingine kisha osha kwa maji ya uvuguvugu.Fanya hivi mara tatu hadi nne kwa siku utapata matokeo mazuri haraka 


2.LIMAO NA BAKING SODA




Jinsi ya kufanya

Kata limao, chota baking soda kijiko kimoja changanya na kipande cha limao. Jipake mchanganyiko huku unasugua maeneo yenye michirizi kwa dakika 10 had I 15.Fanya hivi Mara tatu au zaidi kwa siku utafurahia matokeo

3.MAFUTA YA NAZI 

Jinsi ya kufanya

Paka mafuta ya nazi maeneo yenye michirizi kisha sugua ,paka Mara nyingi uwezavyo kwa siku. Unaweza kuchanganya mafuta ya Nazi na   mafuta ya zaituni(olives oil),mafuta ya alizeti,cocoa butter,shear butter na mafia ya parachichi


4.ALOE VERA (MSHUBIRI)


 Jinsi ya kufanya

 Kata jani aloe vera paka utomvu wake  kwenye  michirizi kisha fugue kwa dakika  10 hadi 15 kisha osha kwa maji  ya uvuguvugu .Baada ya wiki tatu utajifurahia

 ZINGATIA ,katika utunzaji ngozi ili ufanikiwe kunywa maji mengi,mbogamboga na  matunda ni jambo la msingi S Ni  matumaini yangu ukifuata  matumizi Kama nilivyoelekeza utapata matokeo mazuri ndani ya wiki tatu hadi  mwezi.

Tukutane kesho  👋👋👋👋