Karibu katika kijiwe hiki cha MarhabaaZanzibar ili tubadilishane uzoefu kuhusu maisha yetu ya kiafrika, tutakuwa na utunzaji ngozi,mavazi, vyakula ,matukio,upashanaji habari na mtindo wa maisha halisi ya kiafrika hususan Zanzibar Ni matarajio yangu kujifunza zaidi kupitia nyinyi wasomaji wangu,nanyi nina imani hamtakosa cha kujifunza toka kwangu. Karibuni sanaaa
HIVI NI MAPENZI KWELI NDIO YAMEPELEKEA NDOA HII AU KUNA JINGINE???
Siku hizi ndoa za vijana na vikongwe ndio habari ya mujini,najiuliza sipati majibu.Najifariji kujijibu mwenyewe labda mabinti wanataka watu wenye uzoefu wa kulea mke.lol
ZIJUE FAIDA ZA MANJANO KWENYE UREMBO
Hapo zamani tulizoea kuiona manjano jikoni tuu, mchuzi bila manjano au wengine wanaita binzari msosi ulikuwa haujanoga bado. Siku hizi mambo yamebadilika manjano imekuwa kiungo muhimu katika ngozi,bila manjano urembo wako haujakamilika.kwenye meza yako ya vipodozi hakikisha Una kikopo cha manjano.Manjano ninayoongelea hapa ni Ile manjano mbichi haijazimuliwa na sembe.maana unaweza ukanunua manjano kumbe wajanja washakuchezea akili.Manjano halisi tena ile fresh ambayo haijakaa muda mrefu store .Hapa tuzianagalie faida na jinsi ya kufanya kufikia matarajio.
1.Inatibu chunusi
Kutokana na tabia uake ya kupambana na bakteria manjano inauwezo wa kukausha chunusi hasa zile zinazotokana na maambukizi ya bakteria. Kwa wenye ngozi ya mafuta unachanganya manjano na m aji ya waridi na wale wenye ngozi kavu unachanganya manjano na mziwa fresh kisha unapaka usoni kwa nusu saa kisha unaosha na maji ya kawaida
2. Inang'arisha ngozi
Manjano inatabia ya kutoa weusi kwenye ngozi unaotokana na cream,kuungua jua au kufubaa kwa ngozi. Changanya manjano na maji ya waridi kisha sugua sehemu iliyoathirika.
3.Inapunguza mikunjo ya uzee.
Kwa wale wenzangu na miyee "age go" manjano ni kimbilio letu. Inapunguza Ile mistari na mikunjo inayoletwa na umri mkubwa.Unachanganya manjano na mtindi na kupaka kwenye ngozi kwa nusu saa.
4.Inapunguza mafuta
Kwa wenye ngozi ya mafuta manjano inasaidia sana kupunguza uzalishaji we mafuta,hapa mtashanga kidogo, Unakunywa glass moja ya mchanganyiko wa maji na manjano angalau mara mbali kwa wiki. Pia unaweza kuchanganya manjano,limao na maji ya waridi na kupaka usoni kwa dakika 30
5.Inapunguza kasi ya ngozi kuzeeka
Baada ya matumizi ya make up wiki nzima jitahidi mwisho wa wiki uwe unafanya facial ya manjano angalau mara moja,maana manjano husaidia ngozi isichoke haraka na hivyo kupaka mwonekano mzuri wa ngozi yako.

JE LIPS ZAKO ZINAVUTIA HATA USIPOPAKA LIPSTICK???
Watu wanajisahau Sana siku hizi, make up zimekuwa ndio maisha yetu.Tunasahau kuna muda hatupaki make up .Kitu cha kuzingatia make up isiwe ndio wewe ,ndio kila kitu.Hata bila make up unatakiwa uwe unajiamini kuwa ni mrembo wa haja.
Leo tuone urembo wa lips ,jinsi ya kutunza lips.Unahitaji kufanya scrub lips zako Mara kwa Mara ili kuondoa ngozi iliyokufa. Scrub ya lips sio Kama ya uso maana ngozi ya lips in laini name rahisi kupata madhara.
Mahitaji: sukari,mafuta ya nazi na asali
Jinsi ya kufanya : weka mafuta ya Nazi kwenye freezer mpaka yawe magumu wastani, kisha changanya na asali ichanganyike vizuri.malizia kuchanganya na sukari .
Paka kwenye lips zako huku unasugua taratibu.Fanya scrub angalau Mara moja kwa wiki.
Baada ya kutumia scrub yako hifadhi kwenye fridge ili isipoteze ubora

RAFIKI MKIA WA FISI
Hii sio story ya kutunga,ni kweli imetokea, kuna huyu Dada alikuwa na mpenzi wake anaishi Uingereza ,walikuwa mbali ila mapenzi yapo. Mwezi wa kumi mwaka Jana huyu Dada kaenda kumtembea shoga yake,kwa bahati mpenzi wake wa UK akamskype wakaanza kupiga story.Jamaa akamuuliza kwani Leo upo wapi,bibiye akajibu nipo kwa shoga yangu.Jamaa akaomba amuone shogake ili ajiridhishe Kama yupo huko kweli, mdada akaelekeza camera kwa rafiki yake aonwe na mpenzi wake.Baada ya maongezi ya Skype kuisha jamaa akatuma msg kuwa rafiki yake walikuwa wote wakati anaongea amemuona shogake hivyo anaomba mawasiliano yake.Bi Dada akamuiliza shogake Kama yupo tayari kuwasiliana na rafiki wa mpenzi wake,akakubali.Bila hiyana Dada wa watu akatuma namba kwa mpenzi wake ili ampe rafiki yake.
Basi bwana hazijapita hata siku mbili jamaa mwenyewe akajitosa kuwasiliana na shoga wa mpenzi wake(namba aliitaka yeye akasingizia anataka rafiki yake). Siku zinaenda mawasiliano yamepamba moto mpaka kufika mwezi was 12 jamaa akarudi Afrika kimyakimya kaja kumchumbia shoga wa mpenzi wake.Baada ya kumaliza kilichomleta jamaa akamtafuta yule bi dada wa mwanzo akiwa na huyo alomchumbia.Dada hana hili wala lile akajua sweetheart kaja kimya kimya amenisurprise, kufika Kule akakutana na surprise ya kikwelikweli,akatambulishwa na jamaa eti "huyu ndiye aliyenileta,nimekuja kumchumbia" kwa hiyo Mimi na wewe baaasi.Bi Dada hajaamini kajiliza weee .Na hizo convo hapo juu ni kati ya bidada na shogake baada ya sekeseke.
Ungekuwa wewe ungefanyaje?
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)