Mafuta ya nazi pamoja na mambo mengine ni kipodozi asilia kwa ngozi na nywele, hebu tuone matumizi na faida za mafuta ya nazi kama kipodozi cha asili katika ngozi.
1.Lip jelly
Unaweza kutumia mafuta ya nazi kama kilainisha ngozi ya midomo kwa kupaka kiasi kidogo cha mafuta juu ya midomo ya chini na juu mara mbili kwa siku,yaani asubuhi na jioni
2.Kilainisha ngozi (skin softener)
Mafuta ya nazi yanafanya kazi kama lotion au cream zinazotumika kulainisha ngozi,paka mafuta ya nazi katika ngozi kavu na ngumu,mfano unaweza kupaka mafuta ya nazi miguuni hasa kwenye nyayo.Fanya hivyo mara mbili kwa siku
3.Kiondoa Vipodozi (make up remover)
Unaweza kutumia mafuta ya nazi kuondoa make up badala ya kutumia chemicals za kuondolea make up kwenye ngozi
4.Matatizo ya ngozi
Mafuta ya nazi yana msaada mkubwa katika utunzaji wa ngozi dhidi ya madoa, fangasi na hata mipasuko.
pia unaweza kutumia mafuta ya nazi kupunguza weusi katikati ya mapaja kwa kupaka mara kwa mara.